“Chikuzee Hajaacha Muziki, Tulikuwa Studio” Rama K Rapper Amesema

Written by on 11 June 2024

MOMBASAI, Kenya, June 11- Aliyekuwa msanii wa hiphop Rama K Rapper ambaye kwa sasa anajiita Rama Rama baada ya kutangaza kuacha muziki miezi kadhaa iliyopita,ameweza kufunguka rasmi sababu zilimfanya yeye kuacha masuala ya sanaa.

Kupitia mahojiano ya simu na watangazaji wetu kwenye The Rush Hour(YugeBwize na Dullah Wa Ghetto),Rama amesema aliacha muziki baada ya kuona mambo mazuri mbele ambayo asingeyafikia akiwa kwenye muziki.

Hata hivyo,The Father,amesema safari na maisha yake ya muziki yaliisha tangu alipotangaza rasmi. Ikumbukwe kwamba kazi ya mwisho ya Rama itakuwa kolabo yake Mlole Classic japo ni kati ya marapa waliokuwa wakitazamwa na kufuatiliwa sana kwa kuamini kwamba siku moja ataiwakilisha pwani kwenye michano.

‘Chikuzee hawezi kuacha muziki,anatulia tu’ ni maneno ya K Rapper kupitia mahojiano ya siku ya Jumatatu ambapo alifunguka kwamba amekuwa na Chikuzee studio siku chache zilizopita.

Akizungumza, Rama amesema walikuwa wameenda kusalimia ‘mic’ na kuongezea kwamba Chikuzee hajaacha muziki, yuko kwenye mapumziko mafupi tu.

Ikumbukwe kwamba Chikuzee pia alikuwa amefunguka kuacha muziki kisa mambo hayaendi. Tulijaribu kumtafuta Chipesa kwa njia ya simu ila hatukufanikiwa kumpata.

Wasanii wengine ambao walishawahi kutishia kuacha muziki ni akiwemo Jay Melody kutoka Tanzania wakati wa Album yake, Otile Brown aliahidi kuacha muziki endapo Album yake ya Grace isingekuwa kwenye album tano bora Africa.

Hata hivyo,Daddy Sele,Lai,Cannibal,Confuser J ni miongoni mwa majina makubwa ukanda wa pwani ambao waliacha muziki wa kidunia na kuanza kufuatilia na kufanya mitikasi ya kidini

 


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist

Background